Shule ya Sekondari ya Ruhuwiko ni miongoni mwa shule 10 zinazomilikiwa na jeshi la ulinzi la Tanzania (JWTZ).Shule hizo ni :-Airwing Secondary School ,Ali Khamis Camp Secondary School,Jitegemee Secondary School, Kawawa Secondary School,Kigamboni Secondary School,Kizuka Secondary School,Makongo High School,Nyuki Secondary School na Unyanyembe Secondary School. Shule hii ni ya mchanganyiko wa wavulana na wasichana ikiwa ni ya bweni na kutwa kuanzia kidato cha kwanza hadi sita.