NOTE
Hakikisha unaambatanisha matokeo yako ya kidato cha nne na cheti cha kuzaliwa viwe katika mfumo wa pdf. Pia Ambatanisha picha ya mwanafunzi anayeomba kujiunga na shule
Program ya Pre - Form Five itaanza tarehe 15 March 2025 hadi tarehe 06 Juni 2025. Ada ya mpango wa Pre - Form Five kwa kipindi chote ni shilingi 550,000/= tu.
Majina ya wanafunzi watakaochaguliwa kujiunga na kidato cha tano katika shule ya Barbro Johansson mwaka 2025 yatatangazwa kila ijumaa baada ya matokeo ya NECTA kidato cha nne. Wanafunzi watakaochaguliwa watalazimika kuthibitisha kujiunga na shule ili wawekewe nafasi zao.
Hakikisha una ufaulu wa alama C na zaidi katika kila somo la tahsusi unayoomba EGM, HKL, HGK, HGL, HGE, PCM, PCB, CBG, PMC & ECA . Kwa maelezo zaidi tupigie 0757 063 349