Shule ya Sekondari ya Wasichana Bukumbi ilianzishwa tarehe 07.03.1988 chini ya mamlaka ya Shule za kujitegemea Mkoani Mwanza. Ni Shule ya Bweni kwa wasichana tu, ina kidato cha Kwanza hadi cha Sita. Mwaka 1999, Shule ilikabidhiwa kwa Jimbo Kuu Katoliki Mwanza. Askofu Mkuu wa Mwanza ndiye mmiliki wa Shule. Tangu Januari 2004, Masista waafrika Wabenediktini wa Mt. Agnes wamepewa jukumu la kuiendesha Shule hii chini ya Idara ya Elimu ya Jimbo Kuu Katoliki la Mwanza. Jumuia ya Sekondari ya Wasichana Bukumbi inajali na inazingatia kuwawezesha wanafunzi wetu kutumia elimu wanayoipata ili kuwakwamua na ujinga, maradhi na umasikini.