Shule ya Msingi ya Kongowe Adventist (English Medium) ina miundo mbinu mizuri , walimu na walezi mahiri wanaoweza kumsaidia mtoto kupata Elimu inayojitosheleza katika nyanja zote muhimu yaani kiakili, kiroho, kimwili , kijamii na stadi za kazi. Mwanafunzi atahakikishiwa huduma bora za malazi, chakula, ulinzi na usalama. Pia usafiri upo kwa wanafunzi wa kutwa.