Hatuna jengo maalum la kusomea kwa sasa.
Tunatumia vyakula vilivyopendekezwa na wataalamu wa afya na lishe. Vyenye kujenga afya ya mwili na akili. Kifungua kinywa asubuhi (early breakfast), kinywaji kizito wakati wa pumziko fupi (mid-breakfast), chakula cha mchana (lunch), uji wa jioni ( kwa watoto wadogo), na chakula cha jioni (Dinner). Vyakula huandaliwa kwa ustadi na usafi wa hali ya juu. Wanafunzi wa kutwa hupata mid-breakfast na lunch.
Usafiri upo kwa ajili ya wanafunzi wa kutwa. Huhusisha wanafunzi waishio kati ya Mlandizi na Kibamba.
Wanafunzi hujihusisha katika shughuli zingine mbalimbali kulingana na rika, jinsi, mapendeleo (hobbies), na talanta. Mfano wapo wanaojihusisha na uimbaji, kuhubiri, kwata na gwaride, huduma ya kwanza, upimaji afya (BMI), ukambikaji, sanaa, bustani n.k.