Shule ya "ST. MONICA MOSHONO GIRLS SECONDARY SCHOOL" ni ya Kanisa Katoliki na ipo katika Jimbo kuu la Arusha, inamilikiwa na Masista wa Augustino Wamisionari. Shule ni wasichana na ya Bweni. Inachukua wasichana wa Dini na Madhehebu yote. Shule inaendeshwa kwa kufuata miongozo ya kanisa katoliki na taratibu zote za Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi.