Shule ya Sekondari ya Nachingwea ni shule iliyopo kusini mwa Tanzania katika mkoa wa Lindi wilayani nachingwea. Ni shule iliyoanza kutoa masomo ya sekondari mwaka 1989 ikiwa ni moja kati ya shule kongwe katika wilaya ya nachingwea . Pia shule hii imebahatika kuwa na kidato cha tano na cha sita na tahasusi zifuatazo : HGK, HGL, HKL na HGE. Shule ya Nachingwea inafanya vizuri sana kidato cha sita.