JOHN PAUL II KAHAMA SEKONDARI: Ni shule kongwe (1984 – 2023) na ina miundombinu yote. Inapokea wanafunzi jinsia zote kuanzia Kidato cha 1 mpaka cha 6. Inatoa elimu fungamano kwa kuzingatia mahitaji ya kitaaluma, kiroho na kimwili. Ina mabweni kwa ajili ya watoto wa kike na wa kiume. wanafunzi wa kutwa pia wanapokelewa. Shule iko Mtaa wa Mission – Mbulu, wilaya ya Kahama, mkoa wa Shinyanga, umbali wa kilomita 5 tu kutoka katikati ya mji.