Jinsi ya kufanya maombi kujiunga na form I, form V au Primary
1
Ukiwa katika ukurasa wa kwanza www.school.co.tz bofya(click) ONLINE APPLICATION
uweze kuona kwa urahisi shule ambazo unaweza fanya maombi. Hapo utachagua kama ni maombi ya kujiunga na FORM - I, FORM - V au PRIMARY.
2
Bofya jina la shule unayotaka kufanya maombi, kisha ukiwa katika ukurasa wa shule husika bofya Apply
3
Soma maelezo kwa umakini kujua siku ya mwisho kufanya maombi, siku ya usaili(interview), muda na mahali pakufanya usaili, kiwango cha kulipia
fomu ya maombi, pamoja na maelekezo na mahitaji mengine yatakayo itajika na kisha bofya APPLY NOW
4
Utaletewa fomu ya maombi, sehemu ya kwanza ya fomu ni taarifa za mwanafunzi na mzazi/mlezi, jaza taarifa kwa usahihi kisha bofya NEXT
5
Sehemu ya pili ya fomu inahusika na malipo ya fomu ya kujiunga (Application Fee), yanafanyika kwa SELCOM kisha bofya SUBMIT ili uweze kupelekwa kwenye ukurasa wa SELCOM ili uweze kufanya malipo.
6
Ukiwa katika ukurasa wa Selcom, utapa machaguo matatu ya kufanya malipo ambayo "Pay using TanQR", "Pay safely with Your or Credit Card" na "Pay using Mobile Number". Chagua chaguo linalokufaa kufanya Malipo mfano " Pay using Mobile Number"
7
Sasa utaletewa ukurasa kwa ajili ya kufanya malipo ya fomu (Application Fee). Hakikisha jina la mfanyabiashara ni Fourtech Solution Ltd
ambayo ndio kampuni miliki ya huu mfumo wa kufanya malipo ya application online. Chagua njia ya kufanya malipo kwa mfano "Pay Using Moble" na bofya Request PIN on phone.
8
Baada ya kubofya Request PIN on phone angalia simu yako na weka namba ya siri kufanya malipo ya fomu na utapokea uJumbe Malipo yako yamefanikiwa . Sasa utarudishwa tena kwenye Tovuti ya www.school.co.tz
9
Kwenye website www.school.co.tz pia utapokea ujumbe kuonyesha fomu yako imetumwa teyari kama inavyoonekana kwenye picha chini.
10
Download fomu yako na kui'print kwa ajili ya kuja nayo siku yakufanya usaili(interview).
Kwa maelezo zaidi Piga : 0677 094 722
Tunza Muda na Pesa kwa kufanya maombi Online
O'Level Schools In
A'Level Schools Taught
Primary & Nursery
