"Holy Face " ni shule ya msingi ya mchepuo wa Kiingereza(English Medium School). Inamilikiwa na jimbo kuu Katoliki Dodoma na kuendeshwa na Masista wa Mtakatifu Theresia wa Mtoto Yesu wa Bukoa tangu mwaka 2018. Shule hii ina ukubwa wa mita za Mraba 41062. Shule hii imesajiliwa mwaka 2019 kama shule ya msingi kwa namba EM. 17936 na kupata cheti cha usajili.