African Schools ni taasisi ya elimu inayotoa elimu ya awali, msingi na elimu ya Sekondari hadi kidato cha sita. Elimu inayotolewa ni kwa Lugha ya Kiingereza (English Medium). Karibu mzazi/mlezi kwa ajili ya elimu ya mtoto wako ambapo pia utashuhudia yafuatayo: Elimu inayomwezesha mwanafunzi kujua thamani ya kuongoza, kufaulu na kujitolea binafsi kujisomea, kufanya udadisi wa kitaaluma, kujiamini na kutambua thamani ya elimu yake na kuzingatia katika maisha yake.